Date: 
19-12-2019
Reading: 
Isaih 7:10-17

THURSDAY 19TH DECEMBER 2019  MORNING
Isaiah 7:10-17 New International Version (NIV)
10 Again the Lord spoke to Ahaz, 11 “Ask the Lord your God for a sign, whether in the deepest depths or in the highest heights.”
12 But Ahaz said, “I will not ask; I will not put the Lord to the test.”
13 Then Isaiah said, “Hear now, you house of David! Is it not enough to try the patience of humans? Will you try the patience of my God also? 14 Therefore the Lord himself will give you[c] a sign: The virgin[d] will conceive and give birth to a son, and[e] will call him Immanuel.[f] 15 He will be eating curds and honey when he knows enough to reject the wrong and choose the right, 16 for before the boy knows enough to reject the wrong and choose the right, the land of the two kings you dread will be laid waste. 17 The Lord will bring on you and on your people and on the house of your father a time unlike any since Ephraim broke away from Judah—he will bring the king of Assyria.”

God promised to be with His people through their hardships and suffering from the Assyrians. God would give them the strength to recover and the will to return to a life of faith.
God is with us; and He has come in the person of Jesus to redeem us from our sinful nature and restore us to righteousness and reconcile us to himself.


ALHAMISI TAREHE 19 DESEMBA 2019 ASUBUHI                                      ISAYA 7:10-17
10 Tena Bwana akasema na Ahazi akinena,
11 Jitakie ishara ya Bwana, Mungu wako; itake katika mahali palipo chini sana, au katika mahali palipo juu sana.
12 Lakini Ahazi akasema, Sitaitaka, wala sitamjaribu Bwana.
13 Naye akasema, Sikilizeni sasa, enyi nyumba ya Daudi; Je! Ni neno dogo kwenu kuwachosha wanadamu, hata mkataka kumchosha Mungu wangu pia?
14 Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli.
15 Siagi na asali atakula, wakati ajuapo kuyakataa mabaya na kuyachagua mema.
16 Kwa maana kabla mtoto huyo hajajua kuyakataa mabaya na kuyachagua mema, nchi ile, ambayo wewe unawachukia wafalme wake wawili, itaachwa ukiwa.
17 Bwana ataleta juu yako, na juu ya watu wako, na juu ya nyumba ya baba yako, siku zisizokuja bado, tangu siku ile aliyoondoka Efraimu kutoka katika Yuda; yaani, mfalme wa Ashuru.


Mungu aliahidi kuwa na watu wake katika magumu na mateso toka kwa Waashuru. Mungu angewapa nguvu za kusimama, na nia ya kurejea katika maisha ya imani.
Mungu yu pamoja nasi; na amekuja kwa njia ya Yesu kutukomboa kutoka katika asili ya dhambi na kutuhesabia haki, pia kutupatanisha kwake.