Date: 
29-11-2022
Reading: 
Isaya 26:11-15

Hii ni Advent;

Jumanne asubuhi tarehe 29.11.2022

Isaya 26:11-15

[11]BWANA, mkono wako umeinuliwa, lakini hawaoni; lakini watauona wivu wako kwa ajili ya watu wako, nao watatahayari; naam, moto utawala adui zako.

[12]BWANA, utatuamuria amani; maana ni wewe pia uliyetutendea kazi zetu zote.

[13]Ee BWANA, Mungu wetu, mabwana wengine zaidi ya wewe wametumiliki; lakini kwa msaada wako peke yako tutalitaja jina lako.

[14]Wao wamekufa, hawataishi; wamekwisha kufariki, hawatafufuka; kwa sababu hiyo umewajilia, na kuwaangamiza, na kuupoteza ukumbusho wao.

[15]Umeliongeza hilo taifa, BWANA, umeliongeza taifa; wewe umetukuzwa, umeipanua mipaka yote ya nchi hii.

Bwana anakuja tuandae mioyo yetu;

Somo la asubuhi hii ni sehemu ya unabii wa Isaya uliotolewa kabla Israeli hawajaenda uhamishoni Babeli. Isaya anaongelea ukuu wa Mungu ambaye angewaokoa watu wake, na wao kuimba wimbo wa sifa kwa Mungu wao. Anakazia (Isaya) kuwa Bwana ndiye Mwokozi, ambaye atawaoka watu wake, nao watamsifu bila kukoma.

Isaya anajenga picha ya Yesu Kristo mwokozi wa ulimwengu ambaye alikuja kuokoa wanadamu na dhambi zao. Ni Yesu pekee aliyekuja kutuokoa, anayestahili sifa na Utukufu. Yesu huyu aliyekuja kutuokoa, anatuita kumuamini ili akirudi tuurithi uzima wa milele.

Siku njema.