Date: 
07-11-2022
Reading: 
Isaya 57:1-2

Jumatatu asubuhi; 07.11.2022

Isaya 57:1-2

[1]Mwenye haki hupotea, wala hakuna atiaye hayo moyoni; na watu watauwa huondolewa, wala hakuna afikiriye ya kuwa mwenye haki ameondolewa asipatikane na mabaya.

[2]Yeye huingia katika amani; wao hustarehe katika vitanda vyao, kila mtu aendaye katika unyofu wake.

Sisi ni wenyeji wa mbinguni;

Bwana Asifiwe;

Nabii Isaya alileta ujumbe kwa Taifa la Mungu juu ya kutoabudu miungu. Somo tulilosoma linaonesha ambavyo waabuduo miungu hupotea maana hawaliweki neno la Mungu moyoni. Ni mazingira ambayo husababisha watu wasimwamini Mungu wa kweli. Mistari 13 ya kwanza inabeba ujumbe wa kutoabudu miungu, ukifuatiwa na ahadi ya msaada na uponyaji (kuanzia mstari wa 14)

Ujumbe wa kuacha ibada ya miungu ulilenga watu wamwabudu Bwana aliyewakomboa toka utumwani.

Vivyo hivyo, ujumbe huu unakuja kwetu kutukumbusha wajibu wetu wa kumwabudu Mungu wa kweli. Ni kwa kumwabudu Mungu wetu tutaurithi uzima wa milele.

Sisi ni wenyeji wa mbinguni 

Uwe na wiki njema.