Date: 
21-11-2022
Reading: 
Isaya 66:1-8

Jumatatu asubuhi tarehe 21.11.2022

Isaya 66:5-8

[5]Lisikilizeni neno la BWANA, ninyi mtetemekao kwa sababu ya neno lake; Ndugu zenu wawachukiao ninyi, waliowatupa kwa ajili ya jina langu, wamesema, Na atukuzwe BWANA, tupate kuiona furaha yenu; lakini watatahayarika.

[6]Sauti ya fujo itokayo mjini! 

Sauti itokayo hekaluni! 

Sauti ya BWANA awalipaye adui zake adhabu!

[7]Kabla hajaona utungu alizaa; 

Kabla maumivu yake hayajampata, 

Alizaa mtoto mwanamume.

[8]Ni nani aliyesikia neno kama hili? 

Ni nani aliyeona mambo kama haya? 

Je! Nchi yaweza kuzaliwa siku moja? 

Taifa laweza kuzaliwa mara? 

Maana Sayuni, mara alipoona utungu, 

Alizaa watoto wake.

Uzima wa Ulimwengu ujao;

Tumemsoma Nabii Isaya akileta ujumbe wa tumaini kwa watu wa Mungu waliokuwa wakiteseka katika maisha yao. Isaya aliwatia moyo wasiwe na hofu nao wawachukiao, maana Bwana yuko nao. Mstari wa sita unaonesha kuwa sauti ya Bwana ina nguvu kuliko sauti zote, mstari wa nane ukidhihirisha nguvu ya Mungu katika kuokoa watu wake.

Kwanza tufahamu na kuamini kwamba yapo maisha baada ya haya tunayoishi. Maisha hayo hatuwezi kuyafikia bila msaada wa Mungu. Katika somo hili la asubuhi hii, Nabii Isaya anatukumbusha kuwa Bwana yupo nasi katika njia zetu. Isaya anatutia moyo kuwa tukimtegemea Bwana, hakika tutashinda. Ni kweli, tukimwamini na kumtegemea Kristo tunayo hakika ya uzima wa ulimwengu ujao.

Tunakutakia wiki njema yenye ushuhuda na mafanikio katika Kristo. Amina.