Date: 
08-06-2019
Reading: 
James 1:5-11 (Yakobo 1:5-11)

SATURDAY 8TH JUNE 2019 MORNING                          

James 1:5-11 New International Version (NIV)

If any of you lacks wisdom, you should ask God, who gives generously to all without finding fault, and it will be given to you. But when you ask, you must believe and not doubt, because the one who doubts is like a wave of the sea, blown and tossed by the wind. That person should not expect to receive anything from the Lord. Such a person is double-minded and unstable in all they do.

Believers in humble circumstances ought to take pride in their high position. 10 But the rich should take pride in their humiliation—since they will pass away like a wild flower. 11 For the sun rises with scorching heat and withers the plant; its blossom falls and its beauty is destroyed. In the same way, the rich will fade away even while they go about their business.

Let us pray to God for wisdom. We all need wisdom and let us have faith that God will hear and answer our prayers.

We are also urged to be humble and not to trust in earthly riches.  Those who are rich should use their money wisely and not despise the poor.


JUMAMOSI TAREHE 8 JUNI 2019  ASUBUHI                            

YAKOBO 1:5-11

Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa. 
Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. 
Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana. 
Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote. 
Lakini ndugu asiye na cheo na afurahi kwa kuwa ametukuzwa; 
10 bali tajiri kwa kuwa ameshushwa; kwa maana kama ua la majani atatoweka. 
11 Maana jua huchomoza kwa hari, huyakausha majani; ua lake huanguka, uzuri wa umbo lake hupotea; vivyo hivyo naye tajiri atanyauka katika njia zake. 
 

Tumwombe Mungu atupe hekima. Sote tunahitaji hekima kutoka Mungu. Tuombe kwa imani bila kuwa na shaka.

Tusitegemee sana mali na fedha. Matajiri wanapaswa kuwa wanyenyekevu na kusaidia wahitaji bila kuwadharau. Mungu atusaidie kuridhika na vitu tulivyonavyo.