Date: 
06-03-2020
Reading: 
John 5:8 (Yohana 5:8)

FRIDAY 6TH MARCH 2020 MORNING                                                                             

John 5:8 New International Version (NIV)

Then Jesus said to him, “Get up! Pick up your mat and walk.” At once the man was cured; he picked up his mat and walked.

Instead of answering Jesus’ question, “Do you want to be made well?” (John 5:6), the man who has been paralyzed for thirty eight years tries to explain why he can’t get healed, and blames others.

Jesus saw the need and receptive power in him; and in this helplessness situation, he is made well.

God knows our every weaknesses and the situation we are going through. In our needs, let us just ask Him to help and answer us as per His perfect will. Our last words should always be, “Nevertheless not my will, but yours be done” (Luke 22:42).


IJUMAA TAREHE 6 MACHI 2020  ASUBUHI                                                        

YOHANA 5:8

Yesu akamwambia, Simama, jitwike godoro lako, uende.

Badala ya kujibu swali la Yesu, “Je, unataka kuwa mzima?” (Yohana 5:6), mtu huyu aliyekuwa amepooza yapata miaka thelathini na nane, anajaribu kueleza ni kwa nini hajaweza kupona pamoja na kuwalaumu wengine.

Yesu analiona hitaji na ile nguvu ya kupokea uponyaji ndani yake; na katika hali hii ya kukosa msaada, Yesu anamponya.

Mungu anajua madhaifu yetu yote, na hali tunazopitia. Tunapokuwa ni wahitaji, tumwombe atusaidie na kutujibu sawa na mapenzi yake. (Luka 22:42).