Date: 
13-08-2019
Reading: 
John 6:37-40 (Yohana 6:37-40)

TUESDAY 13TH AUGUST 2019 MORNING                                 

John 6:37-40 New International Version (NIV)

37 All those the Father gives me will come to me, and whoever comes to me I will never drive away. 38 For I have come down from heaven not to do my will but to do the will of him who sent me. 39 And this is the will of him who sent me, that I shall lose none of all those he has given me, but raise them up at the last day. 40 For my Father’s will is that everyone who looks to the Son and believes in him shall have eternal life, and I will raise them up at the last day.”

Thank God for these words of encouragement from Jesus Christ Himself. Christ died to save you. Trust in Him. He will protect you and give you Eternal Life. Praise God for your salvation.  


JUMANNE TAREHE 13 AGOSTI 2019 ASUBUHI                       

YOHANA 6:37-40

37 Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe. 
38 Kwa kuwa mimi sikushuka kutoka mbinguni ili niyafanye mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenipeleka. 
39 Na mapenzi yake aliyenipeleka ni haya, ya kwamba katika wote alionipa nisimpoteze hata mmoja, bali nimfufue siku ya mwisho. 
40 Kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho. 


Mshukuru Mungu kwa maneno haya mazuri ya Yesu Kristo. Yesu anakupenda. Yesu alikufa msalabani ili akuokoe. Mtengemee Yesu. Yesu atakulinda na atakupa maisha ya milele. Mshukuru Mungu kwa wokovu wako.