Date: 
06-01-2021
Reading: 
John 8:12-14 (Yohana 8:12-14)

WEDNESDAY 6TH JANUARY 2021 MORNING                                       

John 8:12-14 New International Version (NIV)

12 When Jesus spoke again to the people, he said, “I am the light of the world. Whoever follows me will never walk in darkness, but will have the light of life.”

13 The Pharisees challenged him, “Here you are, appearing as your own witness; your testimony is not valid.”

14 Jesus answered, “Even if I testify on my own behalf, my testimony is valid, for I know where I came from and where I am going. But you have no idea where I come from or where I am going.

Jesus came to open our eyes to the truth. He came to enlighten and show us the way of salvation. Jesus is offering the light that produces eternal life so that whosoever believes on Him by grace through faith, shall be moved from the kingdom of darkness, and placed into God's eternal kingdom of light.


JUMATANO TAREHE 6 JANUARY 2021  ASUBUHI                        

YOHANA 8:12-14

12 Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.
13 Basi Mafarisayo wakamwambia, Wewe unajishuhudia mwenyewe; ushuhuda wako si kweli.
14 Yesu akajibu, akawaambia, Mimi ningawa ninajishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu ndio kweli; kwa sababu najua nilikotoka na niendako; lakini ninyi hamjui nilikotoka wala niendako.

Yesu alikuja kufungua macho yetu ili tuone ile kweli. Amekuja kutuangazia na kutuonesha njia ya wokovu. Yesu anatupa nuru iletayo uzima wa milele ili kwamba yeyote amwaminiye kwa neema, kwa njia ya imani, aokolewe kutoka utawala wa giza na kuingizwa katika ufalme wa nuru wa Mungu.