Date: 
25-05-2020
Reading: 
John 8:13-20

MONDAY 25TH MAY 2020     MORNING                                                                 

John 8:13-20  New International Version (NIV)

13 The Pharisees challenged him, “Here you are, appearing as your own witness; your testimony is not valid.”

14 Jesus answered, “Even if I testify on my own behalf, my testimony is valid, for I know where I came from and where I am going. But you have no idea where I come from or where I am going. 15 You judge by human standards; I pass judgment on no one. 16 But if I do judge, my decisions are true, because I am not alone. I stand with the Father, who sent me. 17 In your own Law it is written that the testimony of two witnesses is true. 18 I am one who testifies for myself; my other witness is the Father, who sent me.”

19 Then they asked him, “Where is your father?”

“You do not know me or my Father,” Jesus replied. “If you knew me, you would know my Father also.” 20 He spoke these words while teaching in the temple courts near the place where the offerings were put. Yet no one seized him, because his hour had not yet come.

 

On the first day of creation, God said, “Let there be light”, and there was light. No matter how dark things may seem in our lives, let us remember that darkness can never overpower light. Let us turn to Christ, the light of the world. He will give us wisdom to perceive Him, patience to wait for Him to remove dark things in our lives; and then power to proclaim His wonderful deeds.


JUMATATU  TAREHE 25 MEI 2020      ASUBUHI                                           YOHANA 8:13-20

13 Basi Mafarisayo wakamwambia, Wewe unajishuhudia mwenyewe; ushuhuda wako si kweli.
14 Yesu akajibu, akawaambia, Mimi ningawa ninajishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu ndio kweli; kwa sababu najua nilikotoka na niendako; lakini ninyi hamjui nilikotoka wala niendako.
15 Ninyi mwahukumu kwa kufuata mambo ya mwili; mimi simhukumu mtu.
16 Nami nijapohukumu, hukumu yangu ni kweli; kwa kuwa mimi si peke yangu, bali ni mimi na yeye aliyenipeleka.
17 Tena katika torati yenu imeandikwa kwamba, Ushuhuda wa watu wawili ni kweli.
18 Mimi ndimi ninayejishuhudia mwenyewe, naye Baba aliyenipeleka ananishuhudia.
19 Basi wakamwambia, Yuko wapi Baba yako? Yesu akajibu, Mimi hamnijui, wala Baba yangu hammjui; kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba yangu.
20 Maneno hayo aliyasema alipokuwa akifundisha hekaluni, katika chumba cha hazina; wala hakuna mtu aliyemkamata, kwa sababu saa yake ilikuwa haijaja bado.

 

Katika siku ya kwanza ya uumbaji, Mungu alisema, “Na iwe nuru”, ikawa nuru. Haijalishi ni mambo mangapi yanaweza kuleta giza katika maisha yetu, tukumbuke kuwa kamwe giza haliwezi kuishinda nuru. Tumgeukie Kristo, yeye aliye nuru ya Ulimwengu. Yesu atatupa hekima ili tumjue yeye, uwezo wa kusubiri ili aondoe mambo ya giza maishani mwetu; na pia atupe nguvu ya kutangaza matendo yake ya ajabu.