Date: 
19-02-2020
Reading: 
John 8:31-36 (Yohana 8:31-36)

WEDNESDAY 19TH FEBRUARY 2020  MORNING                                                      

John 8:31-36 New International Version (NIV)

31 To the Jews who had believed him, Jesus said, “If you hold to my teaching, you are really my disciples. 32 Then you will know the truth, and the truth will set you free.”

33 They answered him, “We are Abraham’s descendants and have never been slaves of anyone. How can you say that we shall be set free?”

34 Jesus replied, “Very truly I tell you, everyone who sins is a slave to sin. 35 Now a slave has no permanent place in the family, but a son belongs to it forever. 36 So if the Son sets you free, you will be free indeed.

Truth is knowledge of God as revealed in Jesus' own self. Knowing this "truth" is to know God.

Without Jesus, we live as slaves. First, we are enslaved to sin, living as oppressed people. Second, this slavery devalues us to inferior status; because of it we cannot claim a permanent place or identity in God's family.


JUMATANO TAREHE 19 FEBRUARI 2020  ASUBUHI                                      

YOHANA 8:31-36

31 Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli;
32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.
33 Wakamjibu, Sisi tu uzao wake Ibrahimu, wala hatujawa watumwa wa mtu wakati wo wote; nawe wasemaje, Mtawekwa huru?
34 Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.
35 Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote.
36 Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.

Kweli maana yake ni kumjua Mungu kama alivyofunuliwa katika Yesu Kristo mwenyewe. Kuijua hii kweli ni kumjua Mungu. Pasipo Yesu, tunaishi kama watumwa: Kwanza, tu chini ya utumwa wa dhambi, tukiishi kama watu wanaoonewa na kuteswa. Pili, utumwa huu unatuondolea thamani yetu na kutufanya tuishi katika hali ya udhaifu; na kwa sababu hiyo hatutambuliki wala kuwa na makao katika familia ya Mungu.