Date: 
17-02-2022
Reading: 
Kutoka 19:3-6

Alhamisi asubuhi tarehe17.02.2022

Kutoka 19:3-6

3 Musa akapanda kwa Mungu, na Bwana akamwita toka mlima ule, akisema, Utawaambia nyumba ya Yakobo, na kuwaarifu wana wa Israeli, maneno haya;

4 Mmeona jinsi nilivyowatendea Wamisri, na jinsi nilivyowachukua ninyi juu ya mbawa za tai, nikawaleta ninyi kwangu mimi.

5 Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu,

6 nanyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu. Hayo ndiyo maneno utakayowaambia wana wa Israeli.

Tunaokolewa kwa neema;

Mungu anawaambia Israeli kupitia kwa Musa kuwa yeye ndiye aliyewakomboa kutoka Misri. Anawaambia kuishi wakimcha yeye, ndipo watakuwa tunu kwake, maana dunia yote ni mali yake. 

Mungu alitaka Israeli watambue kuwa yeye ndiye mkombozi wao, wamche na kumtumikia yeye. Yesu anatutaka tutambue kuwa yeye ndiye mwokozi, akituita kumcha na kumtumikia yeye. Kumcha na kumtumikia ni kutenda mema, tukijiandaa kuurithi uzima wa milele.

Siku njema.