Date: 
21-09-2021
Reading: 
Kutoka 3:7-10

JUMATANO TAREHE 21 SEPTEMBA 2021, ASUBUHI.

Kutoka 3:7-10

BWANA akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao;

8 nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi.

9 Basi, tazama, kilio cha wana wa Israeli kimenifikilia; tena nimeyaona hayo mateso ambayo Wamisri wanawatesa.

10 Haya, basi, nitakutuma sasa kwa Farao, ili upate kuwatoa watu wangu, hao wana wa Israeli, katika Misri.

 

Huruma ya Mungu;

Mungu anamtokea Musa akimwambia kuwa amesikia kilio cha Israeli, hivyo anataka kuwatoa Misri. Hiyo Mungu anampa kazi Musa, pale anapomwambia na kumtuma kwa Farao akawatoe wana wa Israel kutoka Misri na kuelekea nchi ya ahadi.

Mungu alisikia kilio cha Israeli, na mateso waliyopata  akawakomboa. Nasi tunapopitia nyakati ngumu, tukimlilia Bwana anasikia na yuko tayari kutusaidia. Huruma yake hutuokoa na mateso. Hivyo tuendelee kukaa kwake ili huruma yake isiondoke kwetu. Siku njema.

Heri Buberwa


TUESDAY 21ST SEPTEMBER 2021, MORNING

Exodus 3:7-10 (NIV)

The Lord said, “I have indeed seen the misery of my people in Egypt. I have heard them crying out because of their slave drivers, and I am concerned about their suffering. So I have come down to rescue them from the hand of the Egyptians and to bring them up out of that land into a good and spacious land, a land flowing with milk and honey—the home of the Canaanites, Hittites, Amorites, Perizzites, Hivites and Jebusites. And now the cry of the Israelites has reached me, and I have seen the way the Egyptians are oppressing them. 10 So now, go. I am sending you to Pharaoh to bring my people the Israelites out of Egypt.”

Read full chapter

God's mercy;

God appears to Moses telling him that he has heard the cry of Israel, so he wants to bring them out of Egypt. God gives Moses a mission, when he tells him and sends him to Pharaoh to take the Israelites’ out of Egypt onto the Promised Land.

God heard the cry of the children of Israel, and He delivered them from their sufferings. And as we go through difficult times, if we cry out to the Lord, He hears and is ready to help us. His mercy saves us from suffering. So let us continue to abide in him so that his mercy may not depart from us.

Good day.