Date: 
10-02-2022
Reading: 
Kutoka 40:34-38

Alhamisi asubuhi tarehe 10.02.2022

Kutoka 40:34-38


34 Ndipo lile wingu likaifunikiza hema ya kukutania, na huo utukufu wa Bwana ukaijaza maskani.
35 Wala Musa hakuweza kuliingia hema la kukutania, kwa sababu lile wingu lilikaa juu yake, na huo utukufu wa Bwana ukaijaza maskani.
36 Na hapo lile wingu lilipoinuliwa kutoka juu ya maskani, wana wa Israeli wakaenda mbele katika safari zao zote,
37 bali kama lile wingu halikuinuliwa, wakati ule hawakusafiri hata siku ile lilipoinuliwa tena.
38 Kwa maana lile wingu la Bwana lilikuwa juu ya maskani wakati wa mchana, na mlikuwa na moto ndani yake wakati wa usiku, mbele ya macho ya nyumba ya Israeli katika safari zao zote. 

Utukufu wa Mwana wa Mungu;

Maskani ya Israeli yanajawa na Utukufu wa Mungu, na sasa wanaweza kusonga mbele kwa msaada wa Bwana. Wingu la Bwana lilifunika maskani yao, utukufu ukajaa, lilipoinuliwa wakaendelea na safari. 

Kazi zetu tunazozifanya hutusaidia kuendesha maisha yetu, lakini kama kazi zenyewe hazimpi Mungu Utukufu, maisha yetu hayawezi kuwa na utukufu. Sasa kwa sisi tuaminio kwa nini tuwe na misha yasiyompa Mungu Utukufu? Tutafakari kama kazi zetu zinao utukufu wa Mungu, ili maisha yetu yampe Mungu Utukufu. 


Siku njema.