Date: 
26-07-2021
Reading: 
Luka 13:1-5

JUMATATU TAREHE 26 JULAI 2021

LUKA 13:1-5

1 Na wakati uo huo walikuwapo watu waliompasha habari ya Wagalilaya wale ambao Pilato alichanganya damu yao na dhabihu zao.
2 Akawajibu akawaambia, Je! Mwadhani ya kwamba Wagalilaya hao walikuwa wenye dhambi kuliko Wagalilaya wote, hata wakapatwa na mambo hayo?
3 Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo.
4 Au wale kumi na wanane, walioangukiwa na mnara huko Siloamu, ukawaua, mwadhani ya kwamba wao walikuwa wakosaji kuliko watu wote waliokaa Yerusalemu?
5 Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo.

Wema wa Mungu watuvuta tupate kutubu;

Yesu anatoa wito kwetu asubuhi hii, akitupa  uchaguzi wa kutubu au kuangamia. Ni baada ya kuulizwa juu ya baadhi ya wale waliodhurika kwenye mikono ya Pilato, na wale walioangukiwa na ukuta kule Siloamu. Yesu anasema wasidhani wale walikuwa na dhambi kuliko wengine. Kwa yote mawili, Yesu anatoa jibu lile lile;

Luka 13:3,5

[3]Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo.

[5]Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo.

Nini Yesu anatuambia hapa?

Tusiwe wepesi wa kuona wengine ni wenye dhambi, bali tufahamu sisi sote ni wenye dhambi. Hivyo sisi sote tunahitaji kufanya toba. Kinyume chake tutaangamia.

Toba ndilo suluhisho la mwenye dhambi. Toba huturejesha kwa Yesu kwa upya, maana tunapotubu anatusamehe tunakuwa wapya.

Ni wito wangu kwako kuishi maisha ya imani ya kweli, msamaha na toba katika kuuendea ufalme wa Mungu. Maana tukitubu tunakuwa na moyo safi, na ni wenye moyo safi ndio watakaomuona Mungu. Nakutakia wiki njema yenye ushuhuda na mafanikio.