Date: 
20-07-2020
Reading: 
Luke 8:22-25

MONDAY 20TH JULY 2020  MORNING                                                         

Luke 8:22-25 New International Version (NIV)

22 One day Jesus said to his disciples, “Let us go over to the other side of the lake.” So they got into a boat and set out. 23 As they sailed, he fell asleep. A squall came down on the lake, so that the boat was being swamped, and they were in great danger.

24 The disciples went and woke him, saying, “Master, Master, we’re going to drown!”

He got up and rebuked the wind and the raging waters; the storm subsided, and all was calm. 25 “Where is your faith?” he asked his disciples.

In fear and amazement they asked one another, “Who is this? He commands even the winds and the water, and they obey him.”

“With Christ in the boat, you can smile at the storm.” Do you know Jesus Christ and His divine power? If not, don’t wait until the storm hits. Seek Him now, trust Him as your Savior; and your only hope will ever come from Him. 


JUMATATU TAREHE 20 JULAI 2020  ASUBUHI                                             

LUKA 8:22-25

22 Ikawa siku zile mojawapo alipanda chomboni yeye na wanafunzi wake, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng'ambo ya ziwa. Wakatweka matanga.
23 Nao walipokuwa wakienda, alilala usingizi. Ikashuka tufani juu ya ziwa, chombo kikaanza kujaa maji, wakawa katika hatari.
24 Wakamwendea, wakamwamsha, wakisema, Bwana mkubwa, Bwana mkubwa, tunaangamia. Akaamka, akaukemea upepo na msukosuko wa maji, vikakoma; kukawa shwari.
25 Akawaambia, Imani yenu iko wapi? Wakaogopa, wakamaka, wakisema wao kwa wao, Ni nani huyu basi hata anaamuru upepo na maji, navyo vyamtii?

Tukiwa na Yesu Kristo katika chombo, tunaweza kutabasamu wakati tufani inapovuma. Je, unamfahamu Yesu Kristo na nguvu zake kama Mungu? Ikiwa bado, usingoje hadi tufani itakapokujia. Mtafute sasa, mwamini kama mwokozi wako; na tumaini lako pekee litatoka kwake daima.