Date: 
16-03-2021
Reading: 
Luke 9:10-17

TUESDAY 16TH MARCH 2021    MORNING                                           

Luke 9:10-17 New International Version (NIV)

10 When the apostles returned, they reported to Jesus what they had done. Then he took them with him and they withdrew by themselves to a town called Bethsaida, 11 but the crowds learned about it and followed him. He welcomed them and spoke to them about the kingdom of God, and healed those who needed healing.

12 Late in the afternoon the Twelve came to him and said, “Send the crowd away so they can go to the surrounding villages and countryside and find food and lodging, because we are in a remote place here.”

13 He replied, “You give them something to eat.”

They answered, “We have only five loaves of bread and two fish—unless we go and buy food for all this crowd.” 14 (About five thousand men were there.)

But he said to his disciples, “Have them sit down in groups of about fifty each.” 15 The disciples did so, and everyone sat down. 16 Taking the five loaves and the two fish and looking up to heaven, he gave thanks and broke them. Then he gave them to the disciples to distribute to the people. 17 They all ate and were satisfied, and the disciples picked up twelve basketfuls of broken pieces that were left over.

God may not call you to preach to thousands, but if you have tasted His mercy, He does call you to serve Him in some way. He wants to use you to give the Bread of Life to those who are hungry. The requirement is that you see how inadequate you are to do anything for Him. Then, He will use you to help meet the needs of a hurting world.


JUMANNE TAREHE 16 MACHI 2021     ASUBUHI                             

LUKA 9:10-17

10 Basi wale mitume waliporudi walimweleza mambo yote waliyoyatenda; akawachukua, akaenda nao faraghani mpaka mji mmoja uitwao Bethsaida.
11 Na makutano walipojua walimfuata; akawakaribisha, akawa akisema nao habari za ufalme wa Mungu, akawaponya wale wenye haja ya kuponywa.
12 Na jua likaanza kushuka; wakamwendea wale Thenashara, wakamwambia, Uage mkutano, ili waende katika vijiji na mashamba ya kandokando wapate mahali pa kulala na vyakula, maana hapa tulipo ni nyika tupu.
13 Akawaambia, Wapeni ninyi chakula. Wakasema, Hatuna kitu zaidi ya mikate mitano na samaki wawili, tusipokwenda tukawanunulie watu hawa wote vyakula.
14 Kwa kuwa wanaume waliokuwako walipata kama elfu tano. Akawaambia wanafunzi wake, Waketisheni watu kwa safu, kila safu watu hamsini.
15 Wakafanya hivyo, wakawaketisha wote.
16 Akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni akavibariki, akavimega, akawapa wanafunzi wake ili wawaandikie mkutano.
17 Wakala, wakashiba wote; na katika vile vipande vilivyowabakia walikusanya vikapu kumi na viwili.

Mungu anaweza asikuite kuwahubiri maelfu, lakini ikiwa umeonja huruma yake, anakuita kumtumikia kwa njia nyingine. Mungu anapenda kukutumia kuwapa mkate wa uzima wale wenye njaa. Sifa kuu unayohitaji kuwa nayo ni kuona mapungufu uliyo nayo. Ndipo atakapokutumia kusaidia kukutana na mahitaji ya dunia hii yenye maumivu.