Date: 
18-02-2022
Reading: 
Malaki 3:17-18

Ijumaa asubuni tarehe18.02.2022 

Malaki 3:17-18
17 Nao watakuwa wangu, asema Bwana wa majeshi, katika siku ile niifanyayo; naam, watakuwa hazina yangu hasa; nami nitawaachilia, kama vile mtu amwachiliavyo mwanawe mwenyewe amtumikiaye.
18 Ndipo mtakaporudi, nanyi mtapambanua kati ya wenye haki na waovu, na kati ya yeye amtumikiaye Mungu na yeye asiyemtumikia.

Tunaokolewa kwa neema;

Asubuhi hii tunasoma habari za Nabii Malaki akileta ujumbe kwa Taifa la Mungu, kuwa watu wote ni wa kwake, akiahidi kuwalinda na kuwaepusha na uovu wote. Katika kumcha Bwana, nabii Malaki anawasihi kupambanua mambo, wakiacha  uovu na kuchagua kumtumikia BWANA.

Malaki alitangaza neema ya Mungu kwa Taifa lake. Neema hiyo ipo hata leo, ambapo Mungu yuko nasi, tukiokolewa kwa njia ya kifo cha Yesu msalabani. Ni wajibu wetu kuchagua fungu jema, yaani kumtumikia BWANA, tukiacha uovu katika maisha ya imani.
Uwe na siku njema.