Date: 
10-11-2022
Reading: 
Maombolezo 3:31-32

Alhamisi asubuhi tarehe 10.11.2022

Maombolezo 3:31-32

[31]Kwa kuwa Bwana hatamtupa mtu 

Hata milele.

[32]Maana ajapomhuzunisha atamrehemu, 

Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake.

Sisi ni wenyeji wa mbinguni;

Sura ya tatu ya Maombolezo inaongelea upendo wa Mungu ulivyo mkuu kwa watu wote. Katika upendo huo tumesoma kwamba Mungu hamtupi milele mtu yeyote amwaminiye. Yeye atamrehemu kwa wingi wa huruma zake. Bwana ni mwema kwa wote wamtumainio kama tunavyosoma nyuma kidogo;

Maombolezo 3:25

[25]BWANA ni mwema kwa hao wamngojeao, 
Kwa hiyo nafsi imtafutayo.

Maisha tunayoishi ni udhihirisho wa upendo wa Mungu kwetu kwa sababu ya wokovu tuliopewa kwa neema. Tusiipoteze neema hii, tudumu katika upendo wa Mungu tukitenda yatupasayo ili tuwe na mwisho mwema.

Siku njema.

 

Heri Buberwa 

Mlutheri