Date: 
16-07-2020
Reading: 
Mark 1:16-20

THURSDAY 16TH JULY 2020  MORNING         

Mark 1:16-20 New International Version (NIV)

16 As Jesus walked beside the Sea of Galilee, he saw Simon and his brother Andrew casting a net into the lake, for they were fishermen. 17 “Come, follow me,” Jesus said, “and I will send you out to fish for people.” 18 At once they left their nets and followed him.

19 When he had gone a little farther, he saw James son of Zebedee and his brother John in a boat, preparing their nets. 20 Without delay he called them, and they left their father Zebedee in the boat with the hired men and followed him.

Jesus has a plan to have you as His follower, no matter what sin you have done. He let the tax-collectors, the prostitutes, and all the lowest sinners in society become his followers. But one important thing to remember, He did not welcome their sin or allow them to follow Him without changing their lives.


ALHAMISI TAREHE 16 Julai 2020  ASUBUHI    

MARKO 1:16-20

16 Naye alipokuwa akipita kando ya bahari ya Galilaya, akamwona Simoni na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi.
17 Yesu akawaambia, Njoni mnifuate, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu.
18 Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.
19 Akaendelea mbele kidogo, akamwona Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye, nao pia walikuwa chomboni, wakizitengeneza nyavu zao.
20 Mara akawaita, wakamwacha baba yao Zebedayo ndani ya chombo pamoja na watu wa mshahara, wakaenda, wakamfuata.

Yesu anao mpango wa kukuita uwe mfuasi wake, haijalishi umefanya dhambi kiasi gani. Aliwaita watoza ushuru, makahaba na wote waliokuwa hawafai katika jamii, wakamfuata. Lakini jambo moja muhimu tunalopaswa kukumbuka ni hili, hakukaribisha uovu wao au kuwaruhusu kumfuata pasipo kuyabadili maisha yao.