Date: 
12-11-2022
Reading: 
Mathayo 5:5

Jumamosi asubuhi tarehe 12.11.2022

Mathayo 5:5

[5]Heri wenye upole; 

Maana hao watairithi nchi.

Sisi ni wenyeji wa mbinguni;

Umati mkubwa ukiwa unamsikiliza mlimani, Yesu aliendelea kutoa mahubiri yake kuhusu jinsi ya kuingia katika ufalme wa Mungu. Mstari tuliosoma unawaelekeza umati kuwa wapole katika maisha yao ndipo watairithi nchi. Maana yake tofauti na hapo wasingeirithi nchi.

Makutano waliambiwa wawe wapole ili waweze kuifurahia na kuirithi nchi. 

Ujumbe huu unatujia asubuhi ukitualika nasi kuwa wapole. Tuwe wasikivu wanaomfuata Kristo tukiwa na kiasi ili kuurithi ufalme wa Mungu. 

Hatma ya kuurithi ufalme iko mikononi mwako, kuwa mpole.

Jumamosi njema.

 

Heri Buberwa 

Mlutheri