Date: 
19-11-2019
Reading: 
Matthew 13:36-43

TUESDAY 19TH NOVEMBER 2019  MORNING                                           

Matthew 13:36-43 New International Version (NIV)

36 Then he left the crowd and went into the house. His disciples came to him and said, “Explain to us the parable of the weeds in the field.”

37 He answered, “The one who sowed the good seed is the Son of Man. 38 The field is the world, and the good seed stands for the people of the kingdom. The weeds are the people of the evil one, 39 and the enemy who sows them is the devil. The harvest is the end of the age, and the harvesters are angels.

40 “As the weeds are pulled up and burned in the fire, so it will be at the end of the age. 41 The Son of Man will send out his angels, and they will weed out of his kingdom everything that causes sin and all who do evil. 42 They will throw them into the blazing furnace, where there will be weeping and gnashing of teeth. 43 Then the righteous will shine like the sun in the kingdom of their Father. Whoever has ears, let them hear.

Those who accept the message of Jesus Christ find themselves against the forces of darkness. Sometimes they are opposed by their fellows who from the outside would appear like Christians but they are not. However, God knows them; and will keep His elect to the end.


JUMANNE TAREHE 19 NOVEMBA 2019  ASUBUHI                                            

MATAYO 13:36-43

36 Kisha Yesu akawaaga makutano, akaingia nyumbani; wanafunzi wake wakamwendea, wakasema, Tufafanulie mfano wa magugu ya kondeni.
37 Akajibu, akasema, Azipandaye zile mbegu njema ni Mwana wa Adamu;
38 lile konde ni ulimwengu; zile mbegu njema ni wana wa ufalme; na yale magugu ni wana wa yule mwovu;
39 yule adui aliyeyapanda ni Ibilisi; mavuno ni mwisho wa dunia; na wale wavunao ni malaika.
40 Basi, kama vile magugu yakusanywavyo na kuchomwa motoni; ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia.
41 Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi,
42 na kuwatupa katika tanuru ya moto, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
43 Ndipo wenye haki watakapong'aa kama jua katika ufalme wa Baba yao. Mwenye masikio, na asikie.

Wale wanaoipokea habari njema ya Yesu Kristo wanakuwa katika upinzani dhidi ya nguvu za giza. Wakati mwingine wanapingwa na wale ambao kwa nje huonekana kama Wakristo, lakini sivyo walivyo. Hata hivyo, Mungu anawajua; naye atawatunza wateule wake mpaka mwisho.