Date: 
28-11-2022
Reading: 
Nahumu 1:9-14

Hii ni Advent;

Jumatatu asubuhi tarehe 28.11.2022

Nahumu 1:9-14

[9]Mnawaza nini juu ya BWANA? Yeye atakomesha kabisa; mateso hayatainuka mara ya pili.

[10]Kwa maana wangawa kama miiba iliyotatana, na kunyweshwa kana kwamba ni katika kunywa kwao, wataliwa kabisa kama mabua makavu.

[11]Ametoka mmoja kwako, aniaye mabaya juu ya BWANA, atoaye mashauri yasiyofaa kitu.

[12]BWANA asema hivi, Ijapokuwa wana nguvu zilizo timilifu, ijapokuwa ni wengi, hata hivyo watakatwa, naye atapita na kwenda zake. Ingawa nimekutesa, sitakutesa tena.

[13]Na sasa nitakuvunjia nira yake, nami nitakupasulia mafungo yako.

[14]Tena BWANA ametoa amri katika habari zako, ya kwamba asipandwe tena mtu awaye yote mwenye jina lako; toka nyumba ya miungu yako nitakatilia mbali sanamu ya kuchora, na sanamu ya kuyeyusha; nitakufanyia kaburi lako; kwa maana u mbovu.

Bwana anakuja tuandae mioyo yetu;

Nahumu alipewa maono juu ya Ninawi, kuwa Bwana angelipiza kisasi kwa wote ambao wangemuasi. Nahumu analeta ujumbe wa watu kutomuasi Bwana, badala yake kuwaza na kutenda mema. Nahumu anaendelea kuleta habari njema ya wale waaminio kuondolewa mateso, wakimcha na kumtumikia Bwana kwa uaminifu.

Wito wa Nahumu ni Taifa la Mungu kumcha Bwana, ili asije kulipiza kisasi juu yao. Wito huu unaletwa kwetu, tukialikwa kumcha Bwana ili kuiepuka hasira ya Mungu. 

Katika majira haya tunakumbushwa kuwa Yesu alikuja, Yesu yupo, Yesu atarudi kwa mara ya pili. Hivyo tunaitwa kumcha, tukijiandaa na kurudi kwake. Amina.

Uwe na wiki njema.

 

Heri Buberwa 

Mlutheri