Date: 
13-04-2023
Reading: 
Luka 24:36-43

Hii ni Pasaka
Alhamisi Asubuhi | 13.04.2023

Luka 24:36-43
36 Na walipokuwa katika kusema habari hiyo, yeye mwenyewe alisimama katikati yao, akawaambia, Amani iwe kwenu.
37 Wakashituka, wakaogopa sana, wakidhani ya kwamba wanaona roho.
38 Akawaambia, Mbona mnafadhaika? Na kwa nini mnaona shaka mioyoni mwenu?
39 Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe. Nishikenishikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili na mifupa kama mnavyoniona mimi kuwa nayo.
40 Na baada ya kusema hayo aliwaonyesha mikono yake na miguu yake.
41 Basi walipokuwa hawajaamini kwa furaha, huku wakistaajabu, aliwaambia, Mna chakula cho chote hapa?
42 Wakampa kipande cha samaki wa kuokwa.
43 Akakitwaa, akala mbele yao.

----------------------------------------------------------

Tutembee na Yesu mfufuka;

Injili ya Luka huelezea Yesu baada ya kufufuka alivyowatokea watu wawili waliokuwa njiani kuelekea Emmau (Luka 24:13-35). Walikuwa wakiongea habari za Yesu aliyefufuka. Hawakumtambua hadi alipojifunua kwao jioni wakila chakula. Baada ya hapo Yesu alitoweka mbele yao, ndipo wale wawili waliporudi Yerusalemu kuwapasha habari wale wanafunzi kumi na moja.

Somo letu linaanzia hapo, walipoenda kuwapasha habari ndipo Yesu akatokea katikati yao akiwaambia "Amani iwe kwenu". Wote walishtuka, Yesu akawaambia wasiogope maana ni yeye mwenyewe. Yesu aliwaondolea wasiwasi, kwamba alifufuka toka kaburini. Nasi tusiogope, maana Yesu alifufuka kwa ajili yetu. Hivyo tutembee na Yesu mfufuka katika safari yetu ya imani ili tuwe na mwisho mwema.


Uwe na Alhamisi njema.