Date: 
14-04-2023
Reading: 
Mambo ya walawi 26:10-13

Hii ni Pasaka

Ijumaa asubuhi tarehe 14.04.2023

Mambo ya Walawi 26:10-13

10 Nanyi mtakula akiba ya zamani mliyoiweka siku nyingi, tena hayo ya zamani mtayatoa, ili myaweke yaliyo mapya.

11 Nami nitaiweka maskani yangu kati yenu; wala roho yangu haitawachukia.

12 Nami nitakwenda kati yenu, nami nitakuwa Mungu wenu, nanyi mtakuwa watu wangu.

13 Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, niliyewaleta mtoke katika nchi ya Misri, ili msiwe watumwa wao; nami nimeivunja miti ya kongwa lenu, nikawaendesha mwende sawasawa

Tutembee na Yesu mfufuka;

Asubuhi hii tunasoma Bwana akiahidi kuwa na maskani kati ya watu wake, pasipo kuwachukia. Bwana anaahidi kuwa nao, akiendelea kuwa Mungu wao na wao wakiwa watu wake. Mstari wa 13 unakazia kuwa Bwana ndiye aliyewatoa Israeli Misri utumwani, hivyo aliwapenda, akakomboa.

Mungu aliwatoa utumwani Misri watu wake kwa kumtumia Musa. Sisi tumekombolewa kwa njia ya kifo cha Yesu msalabani. Yesu aliyefufuka ndiye anaahidi kuwa nasi, nasi tuwe watu wake. Kufufuka kwake ni tangazo la ushindi wa dhambi. Basi tuzidi kudumu katika imani ya kweli, ili Yesu huyu asiondoke kwetu.

Tutembee na Yesu mfufuka;

 

Heri Buberwa