Date: 
19-04-2023
Reading: 
Waefeso 2:18-22

Hii ni Pasaka

Jumatano asubuhi tarehe 19.04.2023

Waefeso 2:18-22

18 Kwa maana kwa yeye sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Baba katika Roho mmoja.

19 Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu.

20 Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.

21 Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana.

22 Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho.

Yesu Kristo ajifunua kwa wanafunzi wake;

Mtume Paulo anaanza sura ya pili kwa kuwaambia Waefeso kuwa zamani walikuwa wafu, lakini Bwana akawahuisha kwa neema. Angalia anavyoandika;

Waefeso 2:5-6

5 hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema.
6 Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu;

Katika muktadha huo, tunasoma Paulo akiandika kuwa Waefeso wamejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, na Yesu Kristo ndiye jiwe kuu la pembeni. 

Kumbe msingi wa imani yetu ni Yesu Kristo ambaye anajifunua kwetu kama Mwokozi wetu. Tunaalikwa kumwamini siku zote za maisha yetu. Amina.

Siku njema.

 

Heri Buberwa