Date: 
27-04-2023
Reading: 
Kumbukumbu la Torati 33:26-29

Hii ni Pasaka 

Alhamisi asubuhi tarehe 27.04.2023

Kumbukumbu la Torati 33:26-29

26 Hapana aliyefanana na Mungu, Ee Yeshuruni, Ajaye amepanda juu ya mbingu ili akusaidie. Na juu ya mawingu katika utukufu wake.

27 Mungu wa milele ndiye makazi yako, Na mikono ya milele i chini yako. Na mbele yako amemsukumia mbali adui; Akasema, Angamiza.

28 Na Israeli anakaa salama, Chemchemi ya Yakobo peke yake, Katika nchi ya ngano na divai; Naam, mbingu zake zadondoza umande.

29 U heri, Israeli. Ni nani aliye kama wewe, taifa lililookolewa na Bwana! Ndiye ngao ya msaada wako, Na upanga wa utukufu wako; Na adui zako watajitiisha chini yako, Nawe utapakanyaga mahali pao pa juu.

Yesu Kristo ni Mchungaji mwema;

Mungu ndiye atunzaye watu wake, huwafukuza adui toka katikati ya watu wake. Watu wake hukaa salama kwa ulinzi wake. Taifa ambalo linatunzwa na Bwana li heri, maana ni taifa lililookolewa na Bwana. Tunachosoma leo asubuhi ni taifa linalostawi kwa sababu ya kutunzwa na Bwana.

Asubuhi hii tunakumbushwa kuwa sisi kama waaminio mmoja mmoja, familia, jamii na Kanisa kwa ujumla hatuwezi kustawi pasipo kuongozwa na Kristo. Lazima tutunzwe na Yesu mwenyewe, aliye Mchungaji mwema.

Mafanikio yetu yatatokana na kumtegemea Yesu wakati wote. Amina.

Siku njema.

 

Heri Buberwa