MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 11 MEI, 2025
SIKU YA BWANA YA 3 BAADA YA PASAKA
NENO LINALOTUONGOZA NI
NDANI YA YESU KUNA MAISHA MAPYA
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna Mgeni aliyetufikia na cheti.
3. Matoleo ya Tarehe 04/05/2025
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
5. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 04/05/2025 ilikuwa ni washarika 726.
6. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.
7. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
8. Jumapili ijayo tarehe 18/05/2025 ni siku ya Kantate Domino, Mwimbieni Bwana wimbo mpya. Makabila yatakayokuwa tayari kuimba siku hiyo wafike ofisini kujiandikisha.
9. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA
KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 24/05/2025
NDOA HII ITAFUNGWA KKKT MBEZI BEACH KATI YA
-
Bw. Elimsiri Edwin Ngowi na Bi. Evelyne George Biita
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa Matangazo karibu na duka letu la vitabu.
10. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Charles Lyimo
- Upanga: Watatangaziana
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio, Watatangaziana
- Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Jackson Kaale
- Mjini kati: Itakuwa hapa Kanisani jumamosi saa moja kamili asubuhi
- Oysterbay/Masaki: Kwa Mzee na Bibi Aron Ndasiwa
- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bwana na Bibi Itemba
- Kawe,Mikocheni, Mbezi Beach: Kwa Bwana na Bibi Elisha Mushumbusi
11. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.
12. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza.
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.