Sikukuu ya Mavuno 2018

Jumapili ya tarehe 21/10/2018 ilikuwa Sikukuu ya sherehe ya Mavuno ilyofana sana. Ibada iliongozwa na Askofu Dr. Alex Malasusa akisaidiana na Chaplain Mzinga na Mchungaji Mwaipopo. Sherehe ilipambwa na kwaya mbali mbali ikiwemo kwaya ya Upendo toka Moshi, Mkombozi toka Msasani, Umoja na tarumbeta za Azaniafront. Sherehe ilianza kwa maandamano mafupi yakiongozwa na wazee wa kanisa. Washarika walifuata wakiwa na sadaka yao ya mavuno. Baada ya ibada ulifanyika mnada wa mazao na wanyama.