Date: 
22-05-2025
Reading: 
2Samwel 6:1-5

Hii ni Pasaka 

Alhamisi asubuhi tarehe 22.05.2025

2 Samweli 6:1-5

1 Basi Daudi akakusanya tena wateule wote wa Israeli, watu thelathini elfu.

2 Akaondoka Daudi akaenda pamoja na watu wote waliokuwa naye, mpaka Baala wa Yuda, ili kulipandisha kutoka huko sanduku la Mungu lililoitwa kwa jina, naam, jina la Bwana wa majeshi akaaye juu ya makerubi.

3 Wakaliweka sanduku la Mungu juu ya gari jipya, wakalitoa katika nyumba ya Abinadabu, iliyoko kilimani; nao Uza na Ahio wana wa Abinadabu wakaliendesha lile gari jipya.

4 Wakalitoa katika nyumba ya Abinadabu iliyoko kilimani, pamoja na sanduku la Bwana; na huyo Ahio akatangulia mbele ya sanduku.

5 Daudi na nyumba yote ya Israeli wakacheza mbele za Bwana kwa nguvu zao zote, kwa nyimbo, na kwa vinubi, na kwa vinanda, na kwa matari, na kwa kayamba, na kwa matoazi.

Kila mwenye pumzi amsifu Bwana;

Mchakato wa kumfanya Daudi kuwa Mfalme haukuwa mwepesi. Samweli alienda kwa Yese na kuwakuta watoto wake wote, ambao walipitishwa mbele yake na Samweli akasema hakuna ambaye Bwana alimchagua! Samweli alisema Bwana hakumchagua yeyote maana haangalii sura, bali moyo! Ndipo Yese akasema yuko mdogo anachunga kondoo porini, akaletwa na Bwana akamwambia kumpaka mafuta Daudi awe mfalme wa Israeli.

Daudi baada ya kufanywa Mfalme, Yerusalemu ikafanywa makao makuu. Wafilisti walipopata habari za Daudi kuwa Mfalme, wakataka kuivamia Israeli. Daudi tena aliwapiga na kuwashinda. Ndipo katika somo la asubuhi hii Daudi anawakusanya Israeli, analileta sanduku la Agano, anawaongoza Israeli kucheza mbele za Bwana kwa nguvu zote. Daudi aliuona ukuu wa Mungu akawaongoza watu kumsifu. Nasi tumsifu Mungu kwa neema yake kwetu. Amina

Alhamisi njema

Heri Buberwa