Date:
28-05-2025
Reading:
Yohana 17:15-19
Hii ni Pasaka;
Jumatano asubuhi, tarehe 28.05.2025
Yohana 17:15-19
15 Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu.
16 Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.
17 Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.
18 Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni.
19 Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli.
Ndugu wakae pamoja kwa umoja;
Sura ya 17 ya Injili ya Yohana ndiyo sala ndefu aliyosali Yesu, iliyoandikwa. Kwa hiyo somo la asubuhi hii ni sehemu ya sala hiyo. Katika sehemu hiyo ya sala, tunasoma Yesu akiomba watu wake walindwe dhidi ya mwovu. Yesu anaendelea kuomba watu aliokabidhiwa watakaswe kwa kweli ya neno. Yesu anajiweka wakfu mwenyewe kwa ajili ya watu wake ili watakaswe katika kweli.
Ukiiangalia sala ya Yesu inahusu kuwaombea watu wake wakae katika yeye, maana anawaombea kulindwa mbali na mwovu, lakini katika neno la Mungu. Ni Yesu mwenyewe ambaye tukimtumaini anatuweka mbali na mwovu. Kumbe kwa njia ya neno la Mungu na kumtegemea, tunayo nguvu ya kumtangaza Kristo kwa pamoja. Tusiache kukaa pamoja. Amina
Jumatano njema
Heri Buberwa