DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI

MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 16 NOVEMBA, 2025

SIKU YA BWANA YA 2 KABLA YA MAJILIO

NENO LINALOTUONGOZA NI

JIANDAE KWA HUKUMU YA MWISHO

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.

3. Matoleo ya Tarehe 09/11/2025

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 09/11/2025 ni Washarika 726

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.

6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.

7. Kamati ya Afya na Ustawi wa jamii inapenda kuwatangazia kuwa mafundisho ya afya kwa wanafunzi wa kipaimara kwa mwaka wa Kwanza na wa pili yatafanyika tarehe 22/11/2025 kuanzia saa 2.30 asubuhi mpaka saa 8.00 mchana hapa usharikani. Wale waliopata kipaimara kuanzia miaka 3 iliyopita wanakaribishwa kwenye mafundisho haya.

8. Tarehe ya ubarikio kwa watoto wa Kipaimara kwa Kiswahili itakuwa ni tarehe 29/11/2025 na kwa Kingereza itakuwa ni tarehe 06/12/2025. Mavazi kwa wavulana ni Suti nyeusi au suruali nyeusi na shati nyeupe ya mikono mirefu viatu vyeusi. Wasichana gauni jeupe la heshima na viatu vyeupe.

9. NDOA: NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 23/11/2025

SAA 8.00 MCHANA

• Bw. Kingstone Mkony na Bi. Tumaini Gabriel Hatibu

KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 22/11/2025 AMBAYO ITAFUNGWA KANISA KUU LA ST. JOSEPH POSTA KATI YA

• Bw. Arnord Bernald na Bi. Merian Kaleb Kabezi

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.

10. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Kenneth Zebedayo

- Upanga: Kwa Agnes Mziray

- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Dr. na Bibi David Ruhago

- Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Jackson Kaale.

- Mjini kati: Itafanyika jumamosi hapa kanisani saa 1.00 asubuhi

- Oysterbay, Masaki: Kwa Bwana na Bibi Geofrey Mchangila

- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bwana na Bibi Itemba

- Kawe,Mikocheni, Mbezi Beach: Watatangaziana

11. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.

12. Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Pili

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.