Date: 
09-11-2019
Reading: 
Revelations 7:1-8 (Ufunuo 7:1-8)

SATURDAY 9TH NOVEMBER 2019 
Revelation 7:1-8 New International Version (NIV)
1 After this I saw four angels standing at the four corners of the earth, holding back the four winds of the earth to prevent any wind from blowing on the land or on the sea or on any tree. 2 Then I saw another angel coming up from the east, having the seal of the living God. He called out in a loud voice to the four angels who had been given power to harm the land and the sea: 3 “Do not harm the land or the sea or the trees until we put a seal on the foreheads of the servants of our God.” 4 Then I heard the number of those who were sealed: 144,000 from all the tribes of Israel.
5 From the tribe of Judah 12,000 were sealed,
from the tribe of Reuben 12,000,
from the tribe of Gad 12,000,
6 from the tribe of Asher 12,000,
from the tribe of Naphtali 12,000,
from the tribe of Manasseh 12,000,
7 from the tribe of Simeon 12,000,
from the tribe of Levi 12,000,
from the tribe of Issachar 12,000,
8 from the tribe of Zebulun 12,000,
from the tribe of Joseph 12,000,
from the tribe of Benjamin 12,000.

Those who are sealed are all who truly belong to God. Believers are in this privileged position by grace (Romans 11:5). We are not deserving of being sealed by God. By being in Christ we are spiritually protected and no one can harm or destroy our salvation. 


JUMAMOSI TAREHE 9 NOVEMBA 2019  ASUBUHI       UFUNUO   7:1-8
1 Baada ya hayo nikaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za nchi, wakizizuia pepo nne za nchi, upepo usivume juu ya nchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wo wote.
2 Nikaona malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye hai; akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na bahari,
3 akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao.
4 Nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika kila kabila ya Waisraeli, watu mia na arobaini na nne elfu.
5 Wa kabila ya Yuda kumi na mbili elfu waliotiwa muhuri. Wa kabila ya Reubeni kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Gadi kumi na mbili elfu.
6 Wa kabila ya Asheri kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Naftali kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Manase kumi na mbili elfu.
7 Wa kabila ya Simeoni kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Lawi kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Isakari kumi na mbili elfu.
8 Wa kabila ya Zabuloni kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Yusufu kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Benyamini kumi na mbili elfu waliotiwa muhuri.

Wale waliotiwa muhuri ni wote wamwaminio Mungu katika kweli. Tunakubaliwa na Mungu kwa neema tu (Romans 11:5). Hatustahili kutiwa muhuri na Mungu. Tunapokuwa ndani ya Kristo tunapata ulinzi wa kiroho na hakuna anayeweza kuharibu au kuondoa wokovu wetu.