Date: 
23-11-2022
Reading: 
Ufunuo wa Yohana 7:13-17

Jumatano asubuhi tarehe 23.11.2022

Ufunuo wa Yohana 7:13-17

[13]Akajibu mmoja wa wale wazee akiniambia, Je! Watu hawa waliovikwa mavazi meupe ni akina nani? Na wametoka wapi?

[14]Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo.

[15]Kwa hiyo wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, nao wanamtumikia mchana na usiku katika hekalu lake, na yeye aketiye katika kiti cha enzi atatanda hema yake juu yao.

[16]Hawataona njaa tena, wala hawataona kiu tena, wala jua halitawapiga, wala hari iliyo yote.

[17]Kwa maana huyo Mwana-Kondoo, aliye katikati ya kiti cha enzi, atawachunga, naye atawaongoza kwenye chemchemi za maji yenye uhai, na Mungu atayafuta machozi yote katika macho yao.

Uzima wa ulimwengu ujao;

Sura ya saba inaanza kuonesha ufunuo wa Yohana akiona watu 144,000 wa makabila yote ya Israeli waliotiwa mhuri mbele ya kiti cha enzi. Ni picha ya waliomwamini Kristo wakiingia kwenye Utukufu. Somo la asubuhi hii linaonesha watu waliovaa mavazi meupe, ambayo yamefuliwa kwa damu ya mwanakondoo wakiwa mbele ya kiti cha enzi. Yohana anaona watu ambao hawana machozi, wakifurahi milele.

Yohana anafunuliwa kuona watu wakiwa mbele ya kiti cha enzi. Sisi tunaoamini tunaalikwa kujiandaa kusimama mbele ya kiti cha enzi siku itakapowadia. Tukimcha Bwana atafututa machozi tukiingia kwenye furaha ya milele, bali tukitenda mabaya tutaukosa uzima wa milele.

Jumatano njema