Date: 
03-11-2022
Reading: 
Wafilipi 2:12-13

Alhamisi asubuhi tarehe 03.11.2022

Wafilipi 2:12-13

[12]Basi, wapendwa wangu, kama vile mlivyotii sikuzote, si wakati mimi nilipokuwapo tu, bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo, utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka.

[13]Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.

Ushuhuda wetu; Hapa nimesimama;

Mtume Paulo anawaandikia Wafilipi kuwa watii, huku wakidumu katika wokovu aliouleta Yesu. Anawasisitizia kuwa watii wa neno la Mungu ambalo ndilo msingi wa maisha kwa kila aaminiye. Katika kuuishi wokovu huu, kuna mahali Paulo alisema kazi ya ufuasi siyo nyepesi;

2 Timotheo 3:12

[12]Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa.

Tunaalikwa kuishi maisha yanayotafsiri wokovu wetu, ambayo siyo rahisi kuyaishi bila neema ya Mungu. 

Tumtegemee Mungu atendaye kazi ndani yetu, ili tutende kwa mapenzi yake. Tukitenda kwa mapenzi yake tunatenda yanayompendeza, na huo ndiyo ushuhuda wetu mwema kama kundi la waaminio.

Alhamisi njema.