Date: 
27-10-2021
Reading: 
Wagalatia 6:11-16

Jumatano tarehe 27.10.2021, asubuhi. 

Wagalatia 6:11-16

[11]Tazameni ni kwa herufi gani kubwa nimewaandikia kwa mkono wangu mimi mwenyewe!
 
[12]Wote watakao kuonekana ni wazuri kwa mambo ya mwili, ndio wanaowashurutisha kutahiriwa; makusudi wasiudhiwe kwa ajili ya msalaba wa Kristo, hilo tu.
 
[13]Kwa maana hata wao wenyewe waliotahiriwa hawaishiki sheria; bali wanataka ninyi mtahiriwe, wapate kuona fahari katika miili yenu.
 
[14]Lakini mimi, hasha, nisione fahari juu ya kitu cho chote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambao kwa huo ulimwengu umesulibishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu.
 
[15]Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya.
[16]Na wote watakaoenenda kwa kanuni hiyo, amani na iwe kwao na rehema, naam, kwa Israeli wa Mungu.

Tukaze mwendo katika Yesu Kristo;

Mtume Paulo anawaandikia Wagalatia wajitahidi kutoonekana wazuri kwa njia ya mwili tu, bali katika Kristo. Anawasihi kuona fahari katika msalaba, ambao kwa njia yake Yesu alikufa kwa ajili yetu. 

Nasi tujitathmini pia, kama tunaona fahari katika Kristo. Lakini tujue hatutaiona fahari hiyo, kama hatumfuati Kristo katika kweli. Kumwamini na kumfuata Yesu ndiyo njia pekee yenye kuona fahari yake, hatimaye uzima wa milele.

Siku njema.