
|
Usharika wa Azania Front ulipokea ugeni kutoka usharika wa Messiah jimbo la Marquete, Michigan nchini Marekani, waliofika tarehe 12/6/2015 na kuondoka 22/6/2015. Messiah ni Usharika rafiki na usharika wa Azania Front toka miaka ya 90, sharika hizi zimekuwa zikishirikiana kwa ukaribu kabisa hasa katika tamaduni za kutembeleana huku wakiwa na kauli mbiu moja ya kutangaza injili. Wangeni walifanikiwa kutembelea maeneo mbalimbali yanayohusina na kanisa la KKKT pia kutembelea maeneo ya makumbusho Daresalaam na Bagamoyo, na baadae mbuga za wanyama za Tarangire na Serengeti. Wageni hawa walifanikiwa kukutana na vikundi mbalimbali vinavyotoa huduma usharikani Azaniafront kama kwaya, madarasa ya Sunday School ,Pia walifanikiwa kukutana na watu mbalimbali na kubadilishana mawazo kuhusu Neno la mungu sambamba na kushiriki ibada ya nyumba kwa nyumba. |

Vijana Lisa (Kushoto) na Courtney wakifurahia jambo katika ibada ya kwanza.

Mama Elipina Mlaki (kulia) akitoa maelekezo kuhusu darasa la kiswahili la shule ya Jumapili

Mch. Dave Mckenly akishukuru kwa zawadi ya Biblia kubwa aliyokabidhiwa kwa niaba ya Usharika.

Mchungaji Dave akikabidhi zawadi kwa Mwl. Jane Mhina kwa ajili ya watoto wa darasa la kiswahili la shule ya jumapili.

Mch. Dave akionyesha zawadi ya msalaba wa shanga uliotengenezwa na watoto wa Sunday School ya Messiah.

Mchungaji kiongozi wa wageni akiongoza wageni kuwaaga washarika wa Azania Front

Mchungaji kiongozi wa wageni kutoka Usharika wa Messiah Michigan Marekani akifuatilia ibada

Mchungaji mgeni akimuonyesha zawadi mchungaji Mzinga

Mchungaji mgeni akimvisha zawadi ya Skafu Mchungaji Mzinga

Mchungaji mgeni akionyesha zawadi ya Biblia washarika wa Azania Front. Nyuma yake ni Jito, na Mzee George Mnyitafu mwanakamati wa
Uhusiano.

Mchungaji mgeni akisoma neno la shukrani kwa washarika wa Azania Front.

Mchungaji Mzinga akimkabidhi mchungaji mgeni zwadi ya picha ya kanisa baada ya hafla ya chakula cha mchana siku ya kuagana.

Mchungaji Mzinga akimkabidhi mgeni zawadi ya Biblia ya kiswahili. Kulia ni Balozi Bertha Somi, mwanakamati ya Uhusiano.

Chaplain Mzinga akikabidhi moja ya vitabu vya Historia ya miaka mia ya Usharika kwa Mch. Dave kwa niaba ya wageni.

Mchungaji Mzinga akishiriki chakula cha mchana pamoja na wageni

Baadhi ya wenyeji wa wageni nao walishiriki chakula cha Mchana

Mchungaji Mzinga na mzee Swai wakionyesha zawadi ya picha ya jengo la kanisa wageni kabla ya kukabidhiwa

Mgeni akionyesha ishara ya kanisa na watu

Mgeni Lisa akitoa maelezo kuhusu zawadi kwa usharika. Kati ni Katelin, akifuatiwa na Courtney. Nyuma yao ni Prof. Carol.

Mwalimu Stella na watoto wa darasa la kiingereza wakiimba pamoja na wageni walipopita kuwasalimia.

Mwalimu Stella akitoa maelezo kuhusu darasa la kingereza ibada ya asubuhi

Mwanakamati ya Uhusiano, Mama Aida (Kushoto) akishiriki chakula cha mchana pamoja na wageni

Mwanakamati wa Uhusiano mama Aida Mwakisu akiwa katika picha ya pamoja na mgeni

Mzee Swai, Katibu wa kamati ya Uhusiano, akiwa na wageni katika kikao cha mrejesho na wageni.

Mzee Swai akiwa na wageni wakielekea katika madarasa ya sunday school

Kulia ni David Blomquist akifatiwa na Aaron Ndasiwa, aliyekuwa akitafsiri, mwisho ni Mary Lou Blomquist

Wageni wakifurahia chakula cha mchana

Mwl. Mgana (kulia) akiwakaribisha wageni kushiriki zawadi kidogo toka kwa watoto wa darasa la Kiingereza.

Wageni wakiimba na watoto darasa la Kiingereza.

Wageni wakionyesha moja ya zawadi walizotoa kwa usharika. Aliye kushoto ni Mark Paulsen, na kulia ni Prof. Carol

Wageni wakionyesha Ramani ya kanisa lao lilipo huko Michigan, Marekani. kulia ni Dr. David Luoma

Wageni wakisalimia na na walimu wa darasa la kiswahili

Wageni wakishiriki ibada ya Pili. Mwenyeji anayeonekana ni Mzee Elibariki Moshi.

Wageni wakifurahi na watoto wa shule ya Jumapili

Wageni wakitoa baadhi ya zawadi kwa watoto.

Wageni wakiwa katika darasa la kingereza ibada ya asubuhi


Wageni wakiwa na wenyeji katika chakula cha mchana


Wageni wakiimba na watoto

Wageni wakisaliamiana na waalimu wa darasa la Kiswahili

Wanakamati wa kamati ya Uhusiano wakipokea zawadi za usharika kwaniaba ya washarika

Darasa la shule ya jumapili la kiswahili wakiwaimbia wageni.

Watoto wakioneshwa zawadi yao ya msalaba kutoka kwa watoto wa Usharika wa Messiah Marekani

Watoto wakipokea zawadi yao ya msalaba uliotengenezwa na watoto wenzao wa Marekani.

