Date: 
17-11-2022
Reading: 
Yeremia 50:1-5

Alhamisi asubuhi tarehe 17.11.2022

Yeremia 50:1-5

[1]Neno hili ndilo alilosema BWANA, katika habari za Babeli, na katika habari za Wakaldayo, kwa kinywa cha Yeremia, nabii.

[2]Tangazeni katika mataifa, 

Mkahubiri na kutweka bendera; 

Hubirini, msifiche, semeni, 

Babeli umetwaliwa! 

Beli amefedheheka; 

Merodaki amefadhaika; 

Sanamu zake zimeaibishwa, 

Vinyago vyake vimefadhaika.

[3]Maana toka kaskazini taifa linakuja juu yake, litakaloifanya nchi yake kuwa ukiwa; wala hapana mtu atakayekaa humo; wamekimbia, wamekwenda zao, mwanadamu na mnyama pia.

[4]Katika siku hizo, na wakati huo, asema BWANA, wana wa Israeli watakuja, wao na wana wa Yuda pamoja; Wataendelea njiani mwao wakilia, nao watamtafuta BWANA, Mungu wao.

[5]Watauliza habari za Sayuni, na nyuso zao zitaelekea huko, wakisema, Njoni ninyi, mjiunge na BWANA, kwa agano la milele ambalo halitasahauliwa.

Jiandae kwa hukumu ya mwisho;

Ni ujumbe wa Bwana kupitia kwa Nabii Yeremia kwenda Babeli ambapo watu waliacha kumcha Bwana. Walifanya ibada ya sanamu. Bwana alichukia sana akaitangazia Babeli kuwa ukiwa. Bwana aliwaonya kwamba kutomcha yeye kungesababisha Babeli kulia kilio kikuu.

Tujihoji kama maisha yetu ni ibada mbele za Mungu kama anavyotutaka tuenende. Tusipomtanguliza Mungu ibada yetu inakuwa siyo ya kweli, inakuwa ibada ya sanamu. Tusipobadilika na kumfuata Bwana kwa uaminifu atatuangamiza, hivyo tujiandae kwa hukumu ya mwisho.

Siku njema.