MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 19 NOVEMBA, 2017

SOMO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI HUKUMU YA MWISHO.

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.

3. Leo hatutakuwa na kipindi maombi na maombezi hapa usharikani; isipokuwa kipindi hicho kitakuwa siku ya Alhamisi ya tarehe 23/11/2017 saa 11.30 jioni. Lengo la kipindi hiki sio kuombea wenye mahitaji tu, bali ni kujifunza mbinu na nyezo za maisha ya ushindi kupitia neno la Mungu.  Jumapili ijayo tarehe 26.11.2017 saa 10.00 jioni hapa Usharikani kutakuwa na faragha ya maombi ya Kamati ya Misioni na uinjilisti, wajumbe wote wa kamati wanaarifiwa ili wafike na tuanze kwa muda. Aidha wajumbe wa kamati nyingine za baraza wanakaribishwa katika maombi hayo ikiwa ni pamoja na wajumbe wa baraza la Wazee na msharika yeyote atayesukumwa kuungana na Kamati ya Misioni na Uinjilisti katika maombi hayo.  Njooni tumlilie Mungu juu ya Usharika wetu na familia zetu.

4. Ijumaa ya tarehe 15, Desemba 2017, Usharika umeandaa “Tamasha la Uimbaji la Krismas litakaloanza saa 11.30 jioni hadi saa 3:00 usiku. Tamasha litahusisha vikundi vyote vya kwaya hapa usharikani, Kwaya ya watoto wetu wa Shule ya Jumapili na kwaya ya ibada ya Kiingereza. Malengo ya tamasha hilo ni:-

Kuadhimisha Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo,

Vikundi vyote kwa pamoja KUMSHUKURU MUNGU kwa uongozi wake na ulinzi kwa Mwaka wote 2017, na kuomba uongozi wake kwa mwaka 2018.

5. Tarehe 25/11/2017 kutakuwa na kikao  cha vikoba cha Wajane na Wagane saa 3.00 asubuhi. Wajumbe wote mnaombwa  msikose kuhudhuria kikao hicho na kufika kwa wakati.

6. Maadhimisho ya Krismasi Kijimbo yatafanyika tarehe 25.11.2017 katika Mtaa wa Bonyokwa.  Hivyo tunaomba wanawake wote waungane pamoja siku hiyo.  Sare ni Kitenge cha miaka 500 ya matengenezo ya Kanisa. Aidha siku hiyo ya maadhimisho Uongozi wa Jimbo umeandaa kutembelea hospitali ya Ocean Road na Muhimbili, kila Usharika utawakilishwa na wanawake wawili, hivyo tunaomba washarika wenye sabuni, mafuta ya kupaka, dawa ya meno, kanga na n.k walete ofisi ya Parish Worker kwa ajili ya kuwapelekea wagonjwa hao.

7. Jumapili ijayo tarehe 26/11/2017 tutashiriki Chakula cha Bwana.  Washarika tujiandae.

8. Washarika mnaombwa kujaza fomu kwa ajili ya utaratibu mpya wa namba za Bahasha. Wazee watagawa fomu hizo. Unapojaza fomu hii usisahau kujaza namba yako unayotumia sasa. Zoezi hili linaanza leo na litaendelea hadi tarehe 10.12.2017.

9. Uongozi wa Umoja wa vijana unapenda kuwakaribisha vijana na washarika wanaopenda kucheza igizo la Krisimasi la kuzaliwa kwa Bwana Yesu wafike kwenye mazoezi kila  siku ya Jumamosi saa 11.00 jioni.

10. NDOA

NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 02/12/2017

SAA 8.00 MCHANA

Bw. Alpha Edward Mlenga              na     Bi. Tausi Abigail Fadhili Sade

SAA 9.00 ALASIRI

Bw. Philemon B. Mtinangi              na     Bi. Riziki A. Kidagho

 

KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 25/11/2017

SAA 10.00 JIONI

Bw. Andrew Jonathan Mkony         na     Bi. Jacqueline Nassib Ndosi

 

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.

 

11. Ibada za Nyumba kwa Nyumba

  • Upanga: Watatangaziana
  • Kinondoni: Kwa Mama Hilda Lwezaura
  • Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Kwa Bwana na Bibi Kowero
  • Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Kwa Prof. na Bibi W. Matuja
  • Oysterbay/Masaki: Watatangaziana
  • Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Emmanuel Matee.
  • Mjini kati: Watatangaziana
  • Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio: Kwa Bwana na Bibi Peter Mlagha

 

12. Zamu: Zamu za wazee ni Kwanza.

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.