MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 04 AGOSTI, 2024
SIKU YA BWANA YA 10 BAADA YA UTATU
NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI
ENENDENI KWA HEKIMA
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti.
3. Matoleo ya Tarehe 28/07/2024
4. Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV.
6. Kitenge chetu cha kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya shilingi 40,000/=
7. Leo tarehe 04/08/2024 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika tujiandae.
8. Jumapili ijayo tarehe 11/08/2024 ni siku ya ubatizo na kurudi kundini. Washarika watakaohitaji huduma hii wafike ofisini kwa Mchungaji.
9. Usharika utapokea wageni wanakwaya kutoka dayosisi ya ziwa victoria Usharika wa Imani Kwaya ya Agape. Watafika ijumaa ijayo tarehe 09/08/2024. Wataondoka tarehe 12/08/2024 saa kumi jioni kuelekea mwanza. Watapokelewa na wenyeji wao kwaya ya Agape Azania front. Washarika tujiandae kuwapokea na kuwaombea.
10. Ofisi kuu ya Vijana Jimbo la Kati, kwa kushirikiana na Mkuu wa Jimbo Mchg. Frank Kimambo wameandaa Kongamano la Vijana litakalofanyika katika Chuo cha Uhasibu Arusha tarehe 10 Septemba 2024 mpaka tarehe 15 Septemba 2024. Aidha, Dawati la Vijana Makao Makuu Arusha limeandaa Kongamano la Viongozi wa Vijana wa Sharika na Mitaa litakalofanyika Dodoma tarehe 4 Septemba 2024 mpaka tarehe 9 Septemba 2024. Gharama ya mshiriki mmoja kwa Makongamano yote Arusha na Dodoma ni TZS 300,000.00. Jimbo na Dayosisi wamewapa vijana fomu kwa ajili ya kuchangisha kwa washarika. Kwa moyo mkunjufu, Uongozi wa Umoja wa Vijana unaomba washarika kuwaunga mkono katika kukamilisha gharama hizi na kuwawezesha kuhudhuria.
11. Kamati ya Ushirikiano na Habari, imeandaa Dodoso (Questionaire) ili kupata mrejesho wa Jarida la Usharika linatoka kila miezi 3.Lengo ni kuwezesha Kamati kuendelea kuboresha Jarida hilo kulingana na mahitaji ya wasomaji. Hivyo, Kamati inaomba Washarika kujaza dodoso hilo na kurejesha ofisi ya usharika mapema iwezekanavyo. Aidha Jarida na 15 bado linapatikana kwa wanaohitaji. Nakala zipo eneo la Lango Kuu na pia Duka letu la vitabu. Tunatanguliza shukurani kwa ushirikiano wenu.
12. Tarehe 28/09/2024 na 29/09/2024 itakuwa ni sikukuu ya mikaeli na watoto. Hivyo tunaomba vikundi vyote vizingatie sherehe hii muhimu ili tuweze kuwaenzi, kuwatunza na kuwatia moyo watoto wetu kwa kuwachangia chochote ili kufanikisha Sikukuu hii. Mungu awabariki.
13. NDOA: NDOA ZA WASHARIKA
KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 17/08/2024
SAA 9.00 ALASIRI
-
Bw. Solomon Elisa Msuya na Bi. Neema Selemani Shemngwa
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.
14. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Upanga: Kwa Bwana na Bibi Mathew Munisi
- Mjini kati: Kwa Mama Hilda Rwanshane
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bw na Bibi Charles Lyimo
- Kinondoni: Kwa …………………………
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Mujuni Mutembei
- Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa …………………………
- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa …………………………….
- Oysterbay, Masaki: Kwa Bwana na Bibi David Mollel
15. Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Kwanza
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki
.