MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 29 JUNI, 2025

SIKU YA BWANA YA 2 BAADA YA UTATU

NENO LINALOTUONGOZA NI  

WITO WA KUINGIA UFALME WA MUNGU

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna Wageni waliotufikia na cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 22/06/2025

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 22/06/2025 ni Washarika 703. Sunday School 254

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.

6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.

7. Leo tarehe 29/06/2025 tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika karibuni. 

8. Jumapili ijayo tarehe 06/07/2025 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika tujiandae. 

9. Uongozi wa umoja wa Vijana unapenda kuwakaribisha vijana wote kujiunga na timu ya mpira wa miguu kwa ajili ya mashindano ya jimbo, yanayokwenda kwa jina la Kimambo Cup. Pia Kutakuwa na mkesha wa maombi ulioandaliwa na vijana siku ya tarehe 4/7/2025 . Vijana wote mnakaribishwa. Aidha Jimbo limeandaa udiakonia tarehe 14-19/7/2025 vijana wote tunakaribishwa kwa ajili ya huduma hiyo.

10. Tarehe 27/9/25 na 28/9/25 itakuwa ni sikukuu ya Mikaeli na Watoto. Hivyo tunaomba vikundi vyote vizingatie sherehe hii muhimu, ili tuweze kuwaenzi, kuwatunza na kuwatia moyo watoto wetu kwa kuwachangia chochote ili kufanikisha sikukuu hii. Mungu awabariki sana.

11. Shukrani: Jumapili ijayo tarehe 06/07/2025 katika ibada ya saa 4.30 asubuhi,

  • Familia ya Bwana na Bibi James Monyo watamshukuru Mungu kwa Baraka nyingi alizowapa ikiwa ni pamoja na kufikisha miaka 60 ya ndoa yao.

Neno: Zaburi 112, Wimbo: TMW 257(Haya ee Moyo wangu)

11. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 12/07/2025

SAA 5.30 ASUBUHI

  • Bw. Traviss Tariq Adlam na Bi. Vanessa Nashera Senkoro

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa Matangazo karibu na duka letu la vitabu.

12. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Mamkwe
  • Upanga: Kwa Bwana na Bibi Simbo Nkya
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Dr. na Bibi David Ruhago
  • Kinondoni: Kwa Mama Hilda Lwezaula
  • Mjini kati: Itakuwa hapa Kanisani jumamosi saa moja kamili asubuhi
  • Oysterbay/Masaki: Kwa Dr. Malentlema
  • Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bwana na Bibi James Monyo
  • Kawe,Mikocheni, Mbezi Beach: Kwa Askofu na Mama Alex Malasusa. 

13. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.

14. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Pili.  

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.