MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 03 AGOSTI, 2025
SIKU YA BWANA YA 7 BAADA YA UTATU
NENO LINALOTUONGOZA NI
TUNAITWA KUZAA MATUNDA MEMA
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.
3. Matoleo ya Tarehe 27/07/2025
4. Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
5. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 27/07/2025 ni Washarika 697. Sunday School 211
6. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.
7. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
8. Tarehe 27/9/25 na 28/9/25 itakuwa ni sikukuu ya Mikaeli na Watoto. Hivyo tunaomba vikundi vyote vizingatie sherehe hii muhimu, ili tuweze kuwaenzi, kuwatunza na kuwatia moyo watoto wetu kwa kuwachangia chochote ili kufanikisha sikukuu hii. Mungu awabariki sana.
9. Jumamosi ijayo tarehe 09.08.2025 kutakuwa na ibada maalumu ya wazee wetu kuanzia miaka 65 na kuendelea, ibada hii itakayofanyika hapa Usharikani kuanzia saa 3.00 asubuhi ikiambatana na Chakula cha Bwana. Pia baada ya ibada hiyo kutakuwa na mazungumzo. Washarika tuendelee kuiombea ibada hiyo.
10. Wanawake mtaa wetu wa Tabora leo tena wameleta mbogamboga na vitu vingine vya shambani walivyovuna mashambani kwao, vitu hivyo vitauzwa baada ya ibada zote hapo nje. Washarika karibuni kununua mazao fresh kutoka shambani.
11. Leo tarehe 03/08/2025 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika Karibuni.
12. Jumapili ijayo tarehe 10/08/2025 ni siku ya ubatizo wa watoto na kurudi kundini. Watakaohitaji huduma hii wafike ofisini kwa Mchungaji.
13. SHUKRANI: Jumapili ijayo tarehe 10/08/2025 katika ibada ya Kwanza saa 1.00 asubuhi
14. Familia ya Bwana na Bibi Simon Jengo watamshukuru Mungu kwa kutimiza miaka 40 ya ndoa, iliyoifunga hapa Azania Front tarehe 10 Agosti 1985.
Neno: Zaburi 107:1,8, Wimbo: TMW 334: NYOTA YENYE NURU
Ibada ya Tatu saa 4.30 asubuhi
- Familia ya Bwana na Bibi Lazaro Kibiwi watamtolea Mungu shukrani ya pekee kwa kuwa pamoja nao kipindi chote cha kumuuguza Baba yao Mzee Philemon Kibiwi na kumpunzisha katika maisha haya.
Neno: zaburi 23, Wimbo: TMW 149 (Chini ya Bawa lako).
15. Uongozi wa vijana Azania unapenda kuwashukuru vijana wote waliojitokeaza jana kwenye mechi iliyoandaliwa kati ya shabiki wa simba na yanga iliyochezwa pale kiwanja cha sinza vatican, haya yalikuwa mazoezi kwa ajili ya mashindano ya mechi itakayochezwa leo Jumapili tar 3/8/25 pale kiwanja cha shule ya Sekondari Tambaza saa tisa mchana, kati ya Vijana usharika wa Kariakoo na Vijana usharika wa Azania Front ,mashindano hayo yanaenda kwa jina la Kimambo Cup. Washarika wote tunakaribishwa kwenda kuangalia mchezo huo. Mungu awabariki
16. NDOA: NDOA ZA WASHARIKA.
KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 08/08/2025
SAA 6.00 MCHANA
-
Bw. Nicholas Kerya Kisiri na Bi. Irene Adolph Kinyanguli
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa Matangazo karibu na duka letu la vitabu.
17. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mzee Charles Lyimo
- Upanga: Kwa Agnes Mziray
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Mcharo Mlaki
- Kinondoni: Kwa ………………………
- Mjini kati: Itakuwa hapa Kanisani jumamosi saa moja kamili asubuhi
- Oysterbay/Masaki: Kwa Bwana Abdiel Mengi
- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bwana na Bibi James Monyo
- Kawe,Mikocheni, Mbezi Beach: Kwa Eng. na Bibi Zebadiah Moshi
18. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.
19. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza.
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.
,