Date:
02-10-2025
Reading:
Mithali 13:24
Alhamisi asubuhi tarehe02.10.2025
Mithali 13:24
Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe; Bali yeye ampendaye humrudi mapema.
Tuwapende na kuwajali watoto katika Bwana;
Suleimani anasema asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe, lakini ampendaye mwanawe humrudi mapema. Suleimani anaeleza juu ya malezi ya watoto, kwa kutumia lugha ya fimbo. Anasema wazazi wasiache kutumia fimbo, hiyo ni chuki! Yaani usipotumia fimbo unakuwa na chuki maana humpendi mwanao! Kuna mahali anasema fimbo inamuokoa mtoto na kuzimu, maana lengo ni kumfumdisha tabia njema, soma hapa chini;
Mithali 23:13-14
13 Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa. 14 Utampiga kwa fimbo, Na kumwokoa nafsi yake na Kuzimu.Natafsiri andiko la Suleimani leo kama wajibu kwa wazazi kuwalea watoto katika njia sahihi. Wazazi tutenge muda wa kutosha kufuatilia maswala yanayowahusu watoto wetu nyumbani, shuleni na Kanisani. Tukumbuke kwamba tukiwalea watoto vizuri tunajenga familia bora, Kanisa imara na Taifa la kesho. Amina
Alhamisi njema
Heri Buberwa Nteboya
0784 968650