Date: 
15-07-2021
Reading: 
WARUMI 12:9-13 (Romans)

ALHAMISI TAREHE 15/07/2021, ASUBUHI

WARUMI 12:9-13

9 Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema.
10 Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;
11 kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana;
12 kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; katika kusali, mkidumu;
13 kwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni mkijitahidi.

Amri ya Upendo;

Mtume Paulo anaandika juu ya maisha mapya katika Kristo, akitaja sifa za mkristo, kuwa ni yule mwenye pendo lisilo na unafiki. Mkristo katika pendo hilo huuchukia uovu.

Mtume Paulo anatuasa kupendana, tukiheshimiana. Huu ndio utume mwema katika Kanisa la Mungu. Anahimiza pia waaminio kukaa pamoja, katika furaha ya Kristo kwa ibada takatifu.

Asubuhi hii tunakumbushwa kuwa na umoja katika Kristo, ambao msingi wake ni upendo. Upendo unatuweka pamoja, hivyo Kanisa kuwa na nguvu moja ya ushuhuda wa imani ya kweli, maana upendo ndiyo amri kuu. Tupendane,tukae pamoja.


THURSDAY 15TH JULY 2021, MORNING

ROMANS 12:9-13

Love must be sincere. Hate what is evil; cling to what is good. 10 Be devoted to one another in love. Honor one another above yourselves. 11 Never be lacking in zeal, but keep your spiritual fervor, serving the Lord. 12 Be joyful in hope, patient in affliction, faithful in prayer. 13 Share with the Lord’s people who are in need. Practice hospitality.

Read full chapter

Commandment of Love;

The apostle Paul writes about the new life in Christ, mentioning the qualities of a Christian, being one with unfeigned love. The Christian in that loves, hates evil.

The apostle Paul exhorts us to love one another, to respect one another. This is the good mission in the Church of God. He also encourages believers to live together, in the joy of Christ for sacred worship.

This morning we are reminded to be united in Christ, whose foundation is love. Love binds us together, so that the Church may have one power to bear witness to the true faith, for love is the greatest commandment. Let's love each other, let's stay together.