Date: 
07-04-2020
Reading: 
2Corinthians 4:16-18

TUESDAY 7TH APRIL 2020  MORNING   
2 Corinthians 4:16-18 New International Version (NIV)


16 Therefore we do not lose heart. Though outwardly we are wasting away, yet inwardly we are being renewed day by day. 17 For our light and momentary troubles are achieving for us an eternal glory that far outweighs them all. 18 So we fix our eyes not on what is seen, but on what is unseen, since what is seen is temporary, but what is unseen is eternal.

Are you discouraged today? No Christian is immune to discouragement. We all lose heart now and then. Maybe your outer self is wasting away. Perhaps your faith is being tested as never before.
Let us look to the unseen for encouragement." During difficult times, let our spiritual eyes come alive. With eyes of faith we shall see what cannot be seen and get a glorious sight of eternity.


JUMANNE TAREHE 7 APRILI 2020  ASUBUHI                                  
2WAKORINTHO 4:16-18

16 Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku.
17 Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana;
18 tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.


Je, kuna jambo limekukatisha tamaa? Hakuna Mkristo mwenye kinga dhidi ya kukatishwa tamaa. Nyakati zote tunapitia mambo ya kutuhuzunisha. Pengine utu wako wa nje unazidi kuharibika; na pengine imani yako inajaribiwa isivyo kawaida. 
Basi, na tuvitazame visivyoonekana kwa ajili ya kuimarishwa. Katika nyakati za shida, Mungu atayapa uhai macho yetu ya rohoni . Kwa imani tutaona yale yasiyoweza kuonekana na kupata picha ya utukufu ule wa milele.