Event Date: 
12-08-2022

Usharika wa KKKT Kanisa Kuu Azania Front Cathedral mnamo tarehe 1 Julai 2022 uliandaa tamasha la uimbaji lililofanyika usharikani ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 12 ya ushirikiano kati ya jiji la Dar es Salaam, Tanzania na jiji la Hamburg, Ujerumani.

Tamasha hilo lilihudhuriwa na wageni waliowakilisha jiji la Hamburg ambapo kwaya zote za usharika wa Kanisa Kuu zilipata kutumbuiza. Katika Tamasha hilo pia alihudhuria Mchungaji Kiongozi wa Usharika, Mchungaji Charles Mzinga.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wakitoa salaam za jiji la Hamburg, wawakilishi hao walisema wanajivunia kuwa nchini Tanzania ili kusherehekea uhusiano mwema uliopo baina ya majiji hayo mawili.

Katika hatua nyingine, wawakilishi wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani walifanya mazungumzo na ujumbe huo kutoka Hamburg juu ya namna ya kuboresha mahusiano baina ya pande mbili. Mazungumzo hayo yalihudhuriwa na Mchungaji Gwakisa Mwaipopo pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Habari na Uhusiano ya Azania Front Cathedral, Mzee Cuthbert Swai.

---------------------------------

Matukio mbalimbali katika picha wakati wa Tamasha la Uimbaji pamoja na kikao kati ya wawakilishi wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani na wageni kutoka jiji la Hamburg nchini Ujerumani.