Event Date: 
12-08-2022

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, limeandaa utaratibu wa wanawake kuongoza ibada mara moja kwa mwaka, ibada hizi kwa kawaida hufanyika katika majira ya Kwaresma au mwezi Machi ambapo dunia huwa inaadhimisha siku ya wanawake duniani.

Kwa mwaka huu wa 2022, katika Usharika wa KKKT Kanisa Kuu Azania Front Cathedral ibada ilifanyika tarehe 21/3/2022 ambapo wanawake waliongoza ibada zote zilizofanyika usharikani hapo siku hiyo.

Katika ibada iliyofanyika usharika wa Azania Front Cathedral mwaka huu, Parish worker wa Usharika, Fedilia Urassa, alisimamia huduma zote na kuwaongoza wanawake walioshiriki katika

huduma mbalimbali ibadani. Litrugia iliongozwa na Jaqueline Munuo, mahubiri yaliongozwa na Mama Anne Mzinga, na pia watoto wa Shule ya Jumapili waliongoza maombi kwa ajili ya siku ya maombi ya watoto duniani. Huduma zingine zote za ibadani zilizohusu siku hiyo ziliongozwa na wanawake wa usharika.

--------------------------------------

Wanawake wa Usharika katika picha za pamoja mara baada ya ibada iliyofanyika katika Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front Cathedral ambapo, siku hiyo ibada zote ziliongozwa na wanawake.