Date: 
05-02-2020
Reading: 
Ephesians 1:11-14 (Waefeso 1:11-14)

WEDNESDAY 5TH FEBRUARY 2020  MORNING                                       

Ephesians 1:11-14 New International Version (NIV)

11 In him we were also chosen,[e] having been predestined according to the plan of him who works out everything in conformity with the purpose of his will, 12 in order that we, who were the first to put our hope in Christ, might be for the praise of his glory. 13 And you also were included in Christ when you heard the message of truth, the gospel of your salvation. When you believed, you were marked in him with a seal, the promised Holy Spirit, 14 who is a deposit guaranteeing our inheritance until the redemption of those who are God’s possession—to the praise of his glory.

We are saved by the grace of God through faith in Jesus Christ. We do not seek God, He seeks us; and we respond by seeking His ways daily. Because we are accepted, our faith in Christ must be engaged in doing the will of God for His own glory.


JUMATANO TAREHE 5 FEBRUARI 2020  ASUBUHI                         

WAEFESO 1:11-14

11 na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake.
12 Nasi katika huyo tupate kuwa sifa ya utukufu wake, sisi tuliotangulia kumwekea Kristo tumaini letu.
13 Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu.
14 Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake.

Tunaokolewa kwa neema ya Mungu kwa njia ya imani katika Yesu Kristo. Hatumtafuti Mungu, bali yeye anatutafuta; na itikio letu ni kutafuta kujua njia zake kila siku. Kwa sababu Mungu ametukubali, imani yetu katika Kristo ni lazima ihusike katika kutenda mapenzi yake, kwa utukufu wake.