Event Date: 
16-06-2021

Hivi karibuni Kwaya ya Agape inayohudumu katika ibada ya Kiswahili, kila Jumapili saa moja asubuhi katika Usharika wa Kanisa Kuu Azaniafront Cathedral waliwatembelea watoto wenye mahitaji mbalimbali katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuwapa mkono wa faraja.

Watoto walionufaika na ziara hiyo ni wale wenye matatizo ya ugonjwa wa mgongo wazi na wale wenye matatizo ya vichwa vikubwa. Ziara ya kuwatembelea watoto hao ilifanyika tarehe 14/4/2021 ambapo mbali na kupatiwa mahitaji ya siku hadi siku watoto hao pia walipata bima za afya (watoto 56).

Kwaya ya Agape inatoa shukrani kwa washarika wote wa Azaniafront kwa kuchangia vitu mbalimbali vilivyofanikisha zoezi hilo.

Wawakiliishi wa Kwaya ya Agape wakiwa tayari kwa ajili ya kukabidhi vitu mbalimbali kwa watoto wenye uhitaji katika Hosptali ya Taifa Muhimbili.

Mwenyekiti wa kwaya ya Agape Moses Kombe akikabidhi fedha kwa ajili ya kununua bima za afya za watoto 56 wenye matitizo ya mgongo wazi na vichwa vikubwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Wawakiliishi wa Kwaya ya Agape wakiwa tayari kwa ajili ya kukabidhi vitu mbalimbali kwa watoto wenye uhitaji katika Hosptali ya Taifa Muhimbili.

 

Ripoti hii imeandaliwa na: Jane Mhina & Paulin Paul