MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 06 NOVEMBA, 2022    

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI

SISI NI WENYEJI WA MBINGUNI

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 30/10/2022

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu. AlhamisiMaombi na Maombezi saa 11.00 jioni. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. Karibu.

5. Leo tarehe 06/11/2022 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika karibuni.

6. Kamati ya Afya na Ustawi wa jamii inapenda kuwatangazia kuwa mafundisho ya afya kwa wanafunzi wa Kipaimara kwa Mwaka wa Kwanza na wa Pili yatafanyika tarehe 19/11/2022 kuanzia saa 2.30 asubuhi mpaka saa 6.00 mchana hapa Usharikani. Wale waliopata Kipaimara wenye umri wa miaka 15 pia wanakaribishwa kwenye mafundisho haya. Wazazi na Walezi mnaombwa kuandikisha watoto watakaohudhuria kwa Parish Worker ili kufanya maandalizi haya.

7. Jumapili ijayo tarehe 13/11/2022 ni siku ya ubatizo wa watoto wadogo na kurudi kundini. Watakaohitaji huduma hii wafike ofisini kwa Mchungaji.

SHUKRANI - JUMAPILI IJAYO TAREHE 13/11/2022

IBADA YA KWANZA – SAA 1.00 ASUBUHI

Familia ya Bwana na Bibi Moses Kombe watamshukuru Mungu kwa mambo mengi aliyotutendea, ikiwa ni pamoja na kuwalinda walipovamiwa na wezi usiku wa 31/08/2022, Ndoa yao kufikisha miaka miwili na kupata baraka ya watoto!

Neno: Mithali 3:5-6, Wimbo: TMW 418 na Kwaya ya Agape

IBADA YA TATU – SAA 4.30 ASUBUHI

Familia ya Bwana na Bibi Eric Mosha watamshukuru Mungu kwa kufikisha miaka 6 ya Ndoa pamoja na mambo mengine mengi aliyowabariki.

Neno: 2Wafalme 3:17, Wimbo: TMW 295

8. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 26/11/2022 AMBAYO ITAFUNGWA ST. JOSEPH KATI YA

Bw. Clement Makagabila na Bi. Lora-Ester Brown Foi

Matangazo mengine yapo kwenye ubao wa Matangazo.

9. NYUMBA KWA NYUMBA 

- Masaki na Oyserbay: kwa Mama Nisile Mollel

- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Charles Lyimo.

- Upanga: Kwa Bwana na Bibi Kavugha

10. Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.