Date: 
11-11-2022
Reading: 
Mathayo 5:4

Ijumaa asubuhi tarehe 11.11.2022

Mathayo 5:4

[4]Heri wenye huzuni; 

Maana hao watafarijika.

Sisi ni wenyeji wa mbinguni;

Ni maneno yaliyoko katika hotuba maarufu ya mlimani, Yesu akionesha yamfaayo mtu kufanya ili kuingia katika ufalme wa Mungu. Yesu alionesha kuwa waaminio wangepata shida nyingi, lakini faraja ya Mungu ingekuwa kwao. Ndiyo maana akasema Heri wenye huzuni maana watafarijika.

Matatizo tunayopitia yasitufanye kukata tamaa katika njia yetu ya ufuasi. Ni muhimu sana kudumu katika Kristo aliye njia ya kweli ili tusiangamie. Yeye atatushindia yote tukimtegemea ili tufike kwake mbinguni.

Ijumaa njema.